PROJECT TITLE (JINA LA MRADI)

PRIMARY SCHOOL RESULT PROCESSING AND MANAGEMENT SYSTEM (PSRPMS)

MFUMO WA UCHAKATAJI NA USIMAMIZI WA MATOKEO KWA SHULE ZA MSINGI
PSRPMS

Tamko la Tatizo (Problem Statement)

Uchakataji wa matokeo ya wanafunzi katika Mitihani ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa kwa shule za Msingi unategemea kutumia lahajedwali (spreadsheet) au uchakataji wa mikono unaosababisha:

1. Ufikiaji Mdogo (Limited Access)

Faili moja ya lahajedwali haiwezi kufunguliwa na watumiaji wengi kwa wakati mmoja. Hivyo, mtu mmoja akitumia, wengine wanasubiri — hii inachelewesha kazi.

2. Makosa ya Kibinadamu katika Upangaji wa Madaraja na Uingizaji wa Data

Ukokotoaji wa alama kwa mikono huweza kusababisha makosa kama kujumlisha vibaya, kupata wastani usio sahihi, au kuandika namba isiyo sahihi. Hii inaweza kupelekea wanafunzi kupata madaraja yasiyo sahihi.

3. Mchakato Mgumu wa Uchambuzi na Tathmini ya Matokeo ya Kitaifa Darasa la 4 na 7

Kipindi Baraza la Mitihani Tanzania likitangaza matokeo walimu hufanya uchambuzi wa madaraja ya ufaulu wa somo kwa njia ngumu ya kuhesabu na kujumlisha idadi ya wanafunzi wenye ufaulu kwa kila daraja (A,B,C,D,E). Mchakato huu unachukua muda mrefu na wakati mwingine hufanyika kimakosa na kupelekea takwimu zisizosahihi.

4. Makosa ya Kuchapa

Wakati wa kuhamisha alama kutoka karatasi kwenda kwenye kompyuta, mtu anaweza kuchapa namba isiyo sahihi. Mfano: 3O badala ya 30. Kosa dogo kama hili linaweza kubadilisha matokeo ya mwanafunzi kabisa.

5. Michakato ya Utawala Inayotumia Muda Mwingi

Walimu na wasimamizi hutumia muda mwingi kukokotoa alama, kuandaa ripoti za wanafunzi mmoja mmoja, na kukusanya ripoti za ufaulu wa darasa zima. Muda huu ungeweza kutumika kufundisha na kuandalia vipindi vya masomo.

6. Masuala ya Usimamizi na Uhifadhi wa Data

Kumbukumbu za karatasi zinaweza kuharibika, kupotea, au kuharibika kwa maji au moto. Pia ni vigumu kupata data ya miaka iliyopita, na hakuna mfumo wa kuhifadhi nakala (backup) endapo kutatokea janga.

7. Uzalishaji wa Ripoti Usiofaa

Kuandaa ripoti kwa mikono huchukua muda mrefu na mara nyingi ripoti hazifanani kwa muundo kati ya madarasa au mihula. Pia kuna ucheleweshaji wa kutoa matokeo, na ni vigumu kuzalisha ripoti maalum za uchambuzi wa ufaulu.

Hitimisho

Changamoto hizi zote zinaonyesha umuhimu wa mfumo wa kidigitali wa kuchakata na kusimamia matokeo ya wanafunzi katika Mitihani mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi Mkoa — mfumo ambao hupunguza makosa, huokoa muda, na hurahisisha upatikanaji wa taarifa, pia kurahisisha uchambuzi wa Madaraja ya Ufaulu katika Matokeo ya Mitihani ya Kitaifa darasa la nne na saba kwa dakika 1-3 tu.

Kupitia MRADI (MFUMO WA PSRPMS) Tutapata Faida Zifuatazo

Uchakataji wa Haraka

Matokeo yanachakatwa papo hapo — kutoka siku kadhaa hadi Dakika chache. Uchambuzi wa NECTA kwa dakika 1–3.

Usahihi wa 100%

Hakuna makosa ya kibinadamu, fomula zinazoharibika, au kuchapa vibaya. Mfumo hukataa alama zisizo sahihi.

Ufikiaji wa Ngazi Zote

Shule, Kata, Halmashauri, na Mkoa — kila ngazi inaona data inayohusika kwa wakati mmoja.

SMS kwa Wazazi

Wazazi/walezi hupokea matokeo ya watoto wao moja kwa moja kwenye simu — bila kuuliza shuleni.

Uchambuzi wa Kina

Madaraja A–E, ufaulu wa jumla na somo moja moja, ripoti za Excel na PDF — zote kiotomatiki.

Usalama wa Data

Encryption ya SSL/TLS, backup za kila siku, na seva zenye uptime ya 99%+.

Utengenezaji wa CAL

Mfumo una uwezo wa kutenngeneza Fomu ya Mahudhurio.

Utengenezaji wa Mpangilio wa Ukaaji kwa Watahiniwa

Mfumo unatengeneza Mpangilio wa Ukaaji wa Watahiniwa katika Chumba cha Mtihani.

Kwa ufupi: PSRPMS huokoa zaidi ya 85% ya muda, huondoa makosa, na huwafanya wazazi kuwa sehemu ya mafanikio ya watoto wao.

Kwa Nini Tumeacha Excel na Kazi za Mkono?

Njia ya Zamani (Excel / Mkono) Mfumo wa PSRPMS
Siku kadhaa hadi wiki za kuchakata matokeo Uchakataji papo hapo baada ya alama kuingizwa
Makosa ya kibinadamu na fomula zinazoharibika Hesabu za kiotomatiki na Usahihi wa 100%
Ugumu wa kukusanya data shule kwenda mkoa Mfumo wa kati ambapo kila ngazi inaona data
Hakuna mawasiliano ya haraka ya matokeo SMS za matokeo zinatumwa moja kwa moja kwa wazazi

Thamani Kuu za PSRPMS

100%

Usahihi Kamili

Hakuna makosa ya hesabu au fomula potofu. Mfumo hufanya kila kitu kiotomatiki na kukataa alama zisizo sahihi.

85%

Muda Uliookolewa

Inafanya kazi 24/7. Inabadilisha kazi za wiki nzima za walimu kuwa kazi ya saa chache tu.

👪

Ushirikishwaji Wazazi

Huondoa haja ya wazazi kwenda shuleni kuuliza matokeo. Wanapata ripoti kiganjani mwao moja kwa moja.

Uokoaji wa Muda wa 85% (Uchambuzi wa Kina)

Kuingiza matokeo (wanafunzi 50)
Dakika 30-60
Dakika 5-10
Kuchakata na kutoa ripoti
Saa 3-8
Sekunde 2-10
Kukusanya matokeo ya Kata
Siku 3-7
Saa 1
Kutuma matokeo kwa wazazi
Siku 1-3
Dakika 5
Tathmini ya NECTA
Siku 2-5
Dakika 10
Zaidi ya 85% ya muda wa utawala unaokolewa.

Uunganishwaji na NECTA & Uchambuzi wa Ngazi Zote

4

Taifa (NECTA Integration)

Mfumo unavuta taarifa moja kwa moja kutoka NECTA. Inachambua madaraja (A–E) kwa Jinsi za Wanafunzi kwenye Ufaulu wa Jumla na Ufaulu wa Somo Moja moja na kuandaa faili la Excel na PDF.

↑
3

Mkoa

Mwenendo wa ufaulu wa halmashauri zote.

↑
2

Kata & Halmashauri

Kulinganisha ufaulu wa shule zote, kubaini shule bora na zenye changamoto.

↑
1

Shule

Ufaulu wa darasa, somo, na nafasi ya shule kwenye kata/halmashauri.

Ushirikishwaji wa Wazazi Papo Hapo

Matokeo: Mwanao amepata wastani wa A. Nafasi darasani: 3 kati ya 50.

Mawasiliano ya Papo Hapo

Wazazi hupokea alama za mtoto na nafasi yake darasani mara tu uchakataji unapokamilika.

Ufanisi wa Gharama

Huokoa gharama na muda wa shule kuandika na kuchapisha barua za matokeo.

Urahisi kwa Wote

Huondoa msongamano wa wazazi wanaokuja shuleni kuulizia maendeleo ya watoto.

Usalama wa Data Unaoaminika

Usimbaji Fiche (Encryption)

Data zote zinalindwa kwa teknolojia ya SSL/TLS zinaposafiri mtandaoni.

Hifadhi Nakala (Backups)

Mfumo unahifadhi nakala (backup) kila siku kuzuia upotevu wa data za shule.

Kinga ya Makosa

Mfumo haukubali alama chini ya 0 au zaidi ya 50, na hukumbusha ikiwa mwanafunzi amerukwa.

Upatikanaji (Uptime)

Seva zenye uwezo mkubwa zinahakikisha mfumo upo hewani kwa zaidi ya 99%.

Udhibiti wa Ufikiaji (Access Levels Blueprint)

Mtumiaji Anaweza Kufanya ✔ Hana Ruhusa ❌
Mwalimu wa Taaluma Kuingiza alama za mtihani na kuona ripoti za darasa. Kusajili wanafunzi au kuona shule nyingine.
Mkuu wa Shule Kusajili shule, walimu, wanafunzi, na kuona matokeo ya shule yake. Kubadilisha matokeo ya shule nyingine.
Afisa Elimu (Kata/Halmashauri/Mkoa) Kuona matokeo ya ngazi yake yote, kulinganisha shule, na kutoa ripoti. Kuingiza au kubadilisha alama za wanafunzi binafsi.

Hatua 7 za Kutumia Mfumo Huu

Hatua 1
→
Hatua 2
→
Hatua 3
→
Hatua 4
→
Hatua 5
→
Hatua 6
→
Hatua 7
Hatua 1: Usajili wa Shule (Msimamizi wa Mfumo ngazi ya Halmashauri).
Hatua 2: Mkuu wa Shule anasajili Wanafunzi na Walimu.
Hatua 3: Mwalimu wa Taaluma anasajili Mitihani ya Ndani.
Hatua 4: Afisa Elimu Kata anasajili mtihani (Kwa mitihani ya Kata).
Hatua 5: Mtihani unafanyika na Walimu wanaingiza alama.
Hatua 6: Mfumo unachakata papo hapo na Ripoti zinapatikana.
Hatua 7: SMS zinatumwa moja kwa moja kwa wazazi.

PSRPMS inaleta mageuzi makubwa

kwa kuondoa makosa ya Excel, kuhakikisha usahihi wa data, na kuwashirikisha wazazi kwa ufanisi. Kuanzia Januari 2026, huu ni mfumo wako wa kisasa na salama.

Je, shule yako tayari imesajiliwa?

+255 747 593 604 | +255 627 534 192 | +255 629 335 929
psrpms@oursystems.co.tz
Tovuti Rasmi ya Mfumo: https://psrpms.oursystems.co.tz
Ingia Hapa

Timu ya Msaada (Inapatikana muda wowote)

ASANTENI SANA!

Nawashukuru wote kwa ushirikiano wenu, muda wenu, na kwa kunisikiliza kwa makini katika uwasilishaji huu wa Mfumo wa PSRPMS. Ni matumaini yangu kwamba mmeona umuhimu na faida za mfumo huu kwa shule zetu za Msingi.

Tuonane tena katika hatua zijazo za mageuzi ya elimu yetu. Kwa pamoja, tutafanikiwa.

KWAHERINI! MUNGU AWABARIKI NYOTE.